Klabu ya Barcelona, kwa kushirikiana na Nike, imezindua rasmi jezi yao mpya ya nyumbani kwa msimu wa 2026/27, ikiwa na muundo unaochanganya utamaduni wa Catalonia na mwonekano wa kisasa unaovutia mashabiki wa soka duniani.
Jezi hiyo imehifadhi rangi za jadi za Blaugrana huku ikiongeza maandishi (typography) mapya yaliyopata msukumo kutoka sanaa ya Catalan Modernism, mtindo maarufu wa usanifu na ubunifu unaotambulisha historia na utamaduni wa eneo la Catalonia.
Nike imeeleza kuwa muundo huo mpya unalenga kuonyesha utambulisho wa Barcelona ndani na nje ya uwanja, huku ukiheshimu urithi wa klabu na kuleta mwonekano wa kisasa kwa kizazi kipya cha mashabiki.
Uzinduzi wa jezi hiyo tayari umeibua hisia mbalimbali mitandaoni, ambapo mashabiki wengi wameisifu kwa muonekano wake wa kipekee na jinsi ilivyohifadhi utambulisho wa kihistoria wa Barcelona.
Barcelona wanatarajiwa kuitumia jezi hiyo kwa mara ya kwanza rasmi katika maandalizi ya msimu mpya wa 2026/27, huku mashabiki wakisubiri kuona kama itakuwa mwanzo wa mafanikio mapya kwa miamba hiyo ya Hispania..jpg)


Β



