Kuondolewa kwa senegal katika hatua ya 32 bora apo jana kiungo mahili wa taifa ilo Pape Gueye ametoa kauli tata iliyoshtua wapenzi na wadau wengi wa soka .
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram kiungo huyo amechapisha andiko linaloeleza kuwa ikiwa hakutakuwa na mabadiliko yeyote kwenye benchi la timu hiyo basi atasimama kwa muda kutumikia Taifa ilo .
Senegal ilipoteza mchezo huo na kufuta ndoto za kutinga hatua ya 16 bora baada ya kukubali kichapo dhidi ya ubelgiji ambao walitumia dakika tano kukomboa uongozi wa senegal wa mabao mawili kabla ya kuongeza la tatu .
Senegal linakuwa taifa lingine kutokea bara la afrika kuaga mashindano ya WC2026 baada ya Tunisia, Dr Congo, Afrika kusini na Ivory Coast



