Timu ya Taifa ya Hispania imeendelea kuonyesha ubora wake katika Kombe la Dunia 2026 baada ya kuichapa Austria kwa mchezo wa upande mmoja na kutinga hatua ya 16 bora ikiwa na rekodi ya asilimia 100 ya ushindi katika hatua ya makundi. Kikosi cha Luis de la Fuente kilitawala mchezo kuanzia mwanzo hadi mwisho, kikionyesha kiwango cha juu kilichowafanya wengi kukitaja miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.
Nyota wa mchezo alikuwa Mikel Oyarzabal, aliyefunga mabao mawili na kufikisha jumla ya mabao manne pamoja na pasi moja ya bao katika mechi nne za Kombe la Dunia 2026. Mshambuliaji huyo ameendelea kuwa tegemeo kubwa la safu ya ushambuliaji ya Hispania kutokana na kiwango chake bora.
Beki wa kushoto Marc Cucurella naye aliendelea kungβara kwa kutoa pasi mbili za mabao, huku Pedro Porro akiandika historia kwa kufunga bao lake la kwanza kabisa akiwa na timu ya taifa ya Hispania. Ushirikiano wao uliifanya Austria ishindwe kabisa kuhimili kasi ya mashambulizi ya La Roja.
Kwa ushindi huo, Hispania imefuzu hatua ya 16 bora ikiwa na rekodi kamili ya ushindi katika hatua ya makundi na kutuma ujumbe mzito kwa wapinzani wake kwamba ipo tayari kupigania taji la dunia.
Sasa macho yanaelekezwa kwenye mchezo wa Portugal dhidi ya Croatia, ambapo endapo Wareno wataibuka na ushindi, dunia ya soka inaweza kushuhudia pambano kubwa la kihistoria kati ya majirani hao wawili katika hatua ya 16 bora.
Hiyo ikiwezekana, itawakutanisha mastaa wakubwa wa Ulaya katika moja ya mechi zinazosubiriwa kwa hamu zaidi, huku Hispania ikisaka kuendeleza mwendo wake mzuri na Portugal ikijaribu kufungua njia ya kuelekea hatua inayofuata.



