Ureno imefanikiwa kusonga mbele hadi hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia 2026 baada ya ushindi mgumu wa mabao 2-1 dhidi ya Croatia, katika mchezo uliokuwa na presha kubwa na drama ya VAR.
Mechi hiyo iliyopigwa Toronto ilihitaji uamuzi wa dakika za mwisho ili kuamua mshindi, huku Croatia wakiondoka wakiwa na maumivu baada ya kukaribia kulazimisha sare dakika za nyongeza.





