Mafarao wafanikiwa kuandika historia kombe la dunia 2026, wakiwatoa nje Australia

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media β€’ 4th July 2026

Mafarao wafanikiwa kuandika historia kombe la dunia 2026, wakiwatoa nje Australia

Misri imeandika historia mpya baada ya kuiondoa Australia kwa mikwaju ya penalti na kufuzu hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia 2026. Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 na muda wa nyongeza, kabla ya Mafarao kuonyesha utulivu kwenye mikwaju ya penalti na kufanikisha ushindi wa kihistoria.

Misri ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Emam Ashour dakika ya 13, kabla ya Australia kusawazisha dakika ya 55 kupitia bao la kujifunga la Hany. Timu zote zilipambana kwa nguvu katika muda uliobaki lakini zilishindwa kupata bao la ushindi.

Baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare, mikwaju ya penalti ndiyo iliyoamua mshindi, huku Misri wakionyesha umakini mkubwa na kufanikiwa kuibuka washindi dhidi ya Australia.

Ushindi huo umeweka rekodi mpya kwa Misri, kwani ni mara ya kwanza katika historia yao kushinda mchezo wa hatua ya mtoano wa Kombe la Dunia la FIFA. Kikosi kinachoongozwa na kocha Hossam Hassan sasa kimeandika ukurasa mpya katika soka la taifa hilo.

Kwa mafanikio hayo, Misri imefuzu rasmi hatua ya 16 bora na itaingia katika duru inayofuata ikiwa na morali kubwa, huku mashabiki wake wakiamini timu hiyo inaweza kuendelea kufanya makubwa katika mashindano ya mwaka 2026.

More Stories

Mafarao wafanikiwa kuandika historia kombe la dunia 2026, wakiwatoa nje Australia
Mafarao wafanikiwa kuandika historia kombe la dunia 2026, wakiwatoa nje Australia
Today, READ MORE β†’
Jumba la maajabu laiponza Yanga, yatozwa faini Tsh Milioni 100
Jumba la maajabu laiponza Yanga, yatozwa faini Tsh Milioni 100
Today, READ MORE β†’
Kinda Fountain Gate mbioni kutua KRC Genk
Kinda Fountain Gate mbioni kutua KRC Genk
Today, READ MORE β†’
Djigui Diarra amaliza msimu akiwa mfalme wa clean sheets
Djigui Diarra amaliza msimu akiwa mfalme wa clean sheets
Today, READ MORE β†’
Azam Fc yamnasa winga hatari Sc Villa
Azam Fc yamnasa winga hatari Sc Villa
Today, READ MORE β†’
Ahmed Ali atamba: Tukitwaa Kombe la CRDB, tutafanya paredi
Ahmed Ali atamba: Tukitwaa Kombe la CRDB, tutafanya paredi
Today, READ MORE β†’
Madrid wavunja ukimya kuhusu tetesi za kumsajili kiungo wa Chelsea, Enzo fernandez.
Madrid wavunja ukimya kuhusu tetesi za kumsajili kiungo wa Chelsea, Enzo fernandez.
Today, READ MORE β†’
Man United waingia kwenye mazungumzo na winga wa West Ham, wakiendelea kupush kwa Baleba pia.
Man United waingia kwenye mazungumzo na winga wa West Ham, wakiendelea kupush kwa Baleba pia.
Today, READ MORE β†’
Simba waifuata Azam kibabe
Simba waifuata Azam kibabe
Today, READ MORE β†’
Mahrez astaafu kutumikia Algeria , Baada ya Taifa ilo Kuondoshwa Kombe la dunia
Mahrez astaafu kutumikia Algeria , Baada ya Taifa ilo Kuondoshwa Kombe la dunia
Today, READ MORE β†’