Shirikisho la soka nchini TFF limetangaza jopo la waamuzi litakalo simamia mchezo wa fainali ya CRDB FEDERATION CUP unaotarajiwa kupigwa hii leo katika uwanja wa Gombani mjini Pemba.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo , Sifu Amon kutoka Mbeya anatarajiwa kuwa mwamuzi wa kati wa mchezo huo akisaidiwa na Hamdani Saidi na Zawadi Yusuph huku Ahmed Arajiga akitangazwa mwamuzi wa akiba wa mchezo.
Mchezo huo unaokutanisha miamba ya Simba na Azam unatarajiwa kutimua vumbi majira ya saa 11 za jioni huku ukusubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wengi wa soka nchini .



