Afisa habari na msemaji wa Simba Sc Ahmed Ally amewaita wanachama , mashabiki na wadau wa soka wa Timu hiyo apo kesho katika uwanja wa ndege J.K.Nyerere ikiwa ni sehemu ya sherehe za ubingwa wa CRDB FEDERATION CUP.
Ahmed ametoa kauli hiyo baada ya kutamatika kwa mchezo wa fainali ulioshuhudia Simba ikiibuka na ushindi baada kuifunga Azam FC bao Moja kwa sifuri katika mchezo wa fainali.
"Tukutane Kesho wapenzi wa simba saa nne asubuhi pale uwanja wa ndege , kwa ambae anaweza kufika basi tukutane Kesho" amesema Ahmed Ally.



