Timu ya Mbeya city imeibuka na ushindi katika mchezo wa mkondo wa kwanza ( playoffs ) baada ya kuinyuka Tanzania Prison jumla ya mabao mawili kwa sifuri.
Katika mchezo huo uliochezwa katika Dimba la sokoine mkoani Mbeya , mabao ya Mbeya city yamewekwa kimiana na Noushad kabla ya msumari wa pili kuwekwa kimiani dakika za mwisho wa mchezo na Hijjah Shamte.





