Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza kufunguliwa kwa dirisha la Usajili msimu wa 2026/2027 kwa Klabu za Ligi Kuu ya NBC, NBC Championship, First League, Ligi Kuu ya Vijana NBC U20 na Ligi Kuu ya Wanawake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo, dirisha hilo limefunguliwa Julai 6, 2026 na litafungwa Agosti 15, 2026 saa 5:59 usiku.





