Mshambuliaji wa Timu ya taifa Morocco , Ismael Saibari anatajwa kukosa mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Ufaransa utakaochezwa hii Leo , kufuatia kusumbuliwa na jeraha la misuli nyuma ya paja .
Saibari ambae ndie kinara wa mabao katika kikosi Cha Morocco baada ya kufungia Taifa ilo mabao matatu , alipata jeraha hilo katika mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Canada na kuondolewa dakika ya 22 ya mchezo huo .
Akizungumza kuelekea mchezo wa Leo Kocha mkuu wa Morocco , Mohammed Ouahbi amesema mshambuliaji huyo hataweza kucheza mchezo wa Leo lakini atarejea uwanjani ikiwa Taifa ilo litatinga hatua ya nusu fainali.
Mchezo wa Morocco dhidi ya Ufaransa unatajwa kuwa mchezo bora hatua ya robo fainali ambapo unatarajiwa kupigwa majira ya saa tano za usiku wa leo kwa saa za afrika mashariki .