International,Normal News,Fc Barcelona, Atletico Madrid

Lamine Yamal Atamani Julián Álvarez Ajiunge na Barcelona

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
9 Jul 2026
Lamine Yamal Atamani Julián Álvarez Ajiunge na Barcelona

Barcelona imezua mjadala mkubwa baada ya nyota wake, Lamine Yamal, kueleza wazi kuwa angefurahia kumuona mshambuliaji wa Argentina, Julián Álvarez, akijiunga na miamba hiyo ya Catalonia katika dirisha hili la usajili.

Yamal anaamini kuwa Álvarez angeendana kikamilifu na mfumo wa uchezaji wa Barcelona, akitaja uwezo wake wa kucheza nafasi mbalimbali za ushambuliaji, kufanya presha ya juu kwa wapinzani na kufunga mabao muhimu. Kwa mujibu wa winga huyo kijana, Álvarez ni aina ya mchezaji ambaye kila klabu kubwa ingetamani kuwa naye.

"Nadhani Julián Álvarez anaendana vizuri sana na mfumo wa Barcelona. Kila mtu anajua ni mchezaji mkubwa, aina ya mchezaji ambaye kila mmoja anatamani kucheza naye. Sijui hali yake ilivyo kwa sasa, lakini natumaini atajiunga nasi. Tutafurahi sana na tutampokea kwa mikono miwili," amesema Yamal.

Kauli hiyo imeongeza nguvu kwa tetesi zinazoendelea kumhusisha mshambuliaji huyo wa Argentina na Barcelona, huku mashabiki wa Blaugrana wakianza kuota ndoto za kuwaona Álvarez na Yamal wakiongoza safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo msimu ujao.

Mtazamo wa Mwana Xtra: Ikiwa usajili huo utatimia, Julián Álvarez anaweza kuwa nyongeza kubwa kwa Barcelona kutokana na ubora wake, uwezo wa kucheza katika mifumo tofauti na uzoefu wake wa kiwango cha juu. Swali kubwa ni: Je, unaamini Álvarez ndiye mshambuliaji anayehitajika Camp Nou?

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE →
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE →
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE →
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE →
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE →
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE →
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE →
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE →
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE →
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE →