Kiungo wa zamani wa klabu ya Simba , Jean Charles Ahoua anaripotiwa kuwa katika hatua za mwisho kukamilisha taratibu za kuvunja mkataba wake ndani ya klabu ya Cr Belouizadad ya nchini Algeria .
Ahoua ambae alitamba akiwa na wekundu wa msimbazi Simba, amefikia hatua hiyo kutokana na kutopata muda wa kutosha wa kucheza akiwa na miamba hiyo ya nchini Algeria .





