Wizara ya Elimu na Michezo nchini Morocco imekanusha taarifa zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa taifa hilo halijioni kama mwakilishi wa Afrika kwenye Kombe la Dunia.
Morocco imesisitiza kuwa inajivunia asili yake ya Kiafrika na nafasi yake ya kuiwakilisha bara hilo katika michuano ya Kombe la Dunia 2026.
Kupitia taarifa rasmi, serikali hiyo imeeleza kuwa hakuna ushahidi wa kauli iliyodaiwa kutolewa na Waziri Mohamed Saad Berrad kwamba Morocco haiwakilishi Afrika, huku ikiwataka wanahabari kuthibitisha taarifa kabla ya kuzisambaza.
Morocco, ikiwa timu pekee ya Afrika iliyosalia kwenye mashindano hayo, imeendelea kuonyesha fahari ya kubeba matumaini ya bara hilo kwenye hatua za mwisho za Kombe la Dunia.