Matumaini ya Simba SC kumsajili kipa wa timu ya Taifa ya Nigeria, Stanley Nwabali, yamefutika rasmi baada ya kipa huyo kurejea Chippa United . Simba ilikuwa ikimuwania Nwabali tangu alipomaliza mkataba wake na Chippa United miezi saba iliyopita, lakini juhudi za kuinasa saini yake zimegonga mwamba.
Leo Jumapili, Julai 12, 2026, Chippa United imetangaza rasmi kumrejesha kipa huyo na kumkaribisha tena ndani ya kikosi chake. Chippa FC ina furaha kumkaribisha tena Stanley Nwabali.
Baada ya muda ambao amekuwa nje, Nwabali amerejea katika Rasi ya Mashariki na tunamkaribisha sana. Nwabali anatajwa kuwa miongoni mwa makipa bora barani Afrika katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kiwango chake bora akiwa na timu ya Taifa ya Nigeria na katika michuano mbalimbali ya kimataifa.
Kwa hatua hiyo, Simba SC italazimika kuendelea kutafuta chaguo jingine la kipa kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya wa mashindano.