Klabu ya Young Africans (Yanga) imeondolewa rasmi marufuku ya usajili iliyokuwa imewekewa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), hatua inayoiruhusu klabu hiyo kusajili wachezaji wapya kuelekea msimu wa 2026/27. Uamuzi huo unakuja baada ya Yanga kukamilisha masharti yote yaliyokuwa yameelekezwa na FIFA kuhusu mgogoro wa kifedha uliokuwa ukiikabili klabu hiyo.





