Klabu ya Yanga SC imethibitisha kuwa maandalizi yake ya msimu wa 2026/27 yatafanyika katika kambi ya Avic Town, huku ikieleza kuwa hakutakuwa na safari ya kwenda nje kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya.
Akizungumza kuhusu maandalizi hayo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe, amesema uongozi wa klabu umefanya tathmini ya ratiba iliyopo na kuamua kubaki Avic Town kutokana na muda mfupi uliobaki kabla ya kuanza kwa mashindano ya msimu mpya.
"Pre-season yetu mwaka huu tunabakia pale pale Avic Town. Hakutakuwa na safari ya kwenda popote kutokana na muda uliobakia," amesema Kamwe.
Kauli hiyo inaweka wazi kuwa kikosi cha Wananchi kitaendelea na programu zake zote za maandalizi katika kambi hiyo, ambapo benchi la ufundi litakuwa na nafasi ya kuwaunganisha wachezaji wapya na wale waliobaki kikosini, sambamba na kuboresha mbinu na utimamu wa mwili kuelekea msimu ujao.
Yanga inaendelea na maandalizi ikiwa na malengo ya kutetea mafanikio yake kwenye mashindano ya ndani na kufanya vizuri zaidi katika michuano ya kimataifa ya CAF, huku mashabiki wakisubiri
Mabingwa hao wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa misimu mitano mfululizo wanatarajiwa kuingia kambini Julai 20