Licha ya msimu uliopita kuhakikisha Mashujaa Fc inasalia kwenye ligi kuu ya NBC, kocha mkuu wa timu hiyo Jamhuri Kiwhelo 'Julio' hatma yake iko mashakani.
Taarifa kutoka chanzo cha uhakika imebainisha kuwa Mashujaa Fc wako sokoni kutafuta kocha mpya ambaye atachukua mikoba ya Julio.
Mashujaa Fc wamefanya mazungumzo na kocha wa Kagera Sugar Juma Kaseja ambaye hata hivyo waajiri wake wameweka ngumu kumuachia.
Baada ya kumkosa Kaseja, Mashujaa Fc sasa wamegeukia kwa Mecky Mexime ambaye hana timu tangu alipoachana na Mbeya City msimu uliopita.
Maafande hao pia wamefanya mazungumzo na kocha wa zamani wa Dodoma Jiji,Amani Richard Josiah.
Inaelezwa mkataba wa Julio na Mashujaa Fc ulimalizika mwishoni mwa msimu uliopita na hakuna mazungumzo yaliyofanyika kuhuisha mkataba wakati timu hiyo ikitarajiwa kuingia mazoezini hivi karibuni kuanza maandalizi ya msimu mpya.