Usajili wa Kelvin Nashon unaonekana kuwa hatua ya Simba SC kuimarisha zaidi safu ya kiungo baada ya miaka ya mafanikio ya Mzamiru Yassin.
Ingawa Mzamiru ameondoka akiwa mmoja wa viungo bora kuwahi kuitumikia Simba, Nashon anaingia akiwa na sifa zinazomfanya aonekane kama upgrade katika baadhi ya maeneo ya kiufundi na kimwili.
MZAMIRU YASSIN
Aliitumikia Simba kwa takribani miaka 10, alicheza zaidi ya mechi 250 katika mashindano yote, alishinda mataji kadhaa ya Ligi Kuu Tanzania, Kombe la FA na Ngao ya Jamii, aliisaidia Simba kufika robo fainali ya CAF Champions League (2021).
Alijulikana kwa nidhamu kubwa uwanjani, uzoefu na uongozi, uwezo wa kukaba na kuzuia mashambulizi, kushinda mipira ya pili na kucheza kwa kujituma dakika zote 90.
KELVIN NASHON
Ni kiungo mwenye umri mdogo na nafasi kubwa ya kuendelea kukua.
Ana uwezo mkubwa wakubeba mpira kutoka nyuma kwenda mbele (ball progression), ushinda mipambano ya mmoja dhidi ya mmoja, kukaba kwa nguvu na kufanya high pressing, kupiga pasi za mbele zinazovunja mistari ya wapinzani, kufunika eneo kubwa kutokana na kasi na nguvu alizonazo.
Kelvin Nashon anaingia Simba akiwa na nguvu zaidi kimwili, kasi kubwa ya mchezo na uwezo wa kuchangia mashambulizi kuliko Mzamiru katika hatua hii ya kazi zao. Wakati Mzamiru alikuwa tegemeo kwa uzoefu na utulivu wake, Nashon analeta nguvu mpya, ubunifu wa kusogeza mpira mbele na uwezo wa kucheza mfumo wa kisasa unaohitaji presha kubwa dhidi ya wapinzani.
Kwa mantiki hiyo, Simba haijapata tu mbadala wa Mzamiru Yassin, bali imepata kiungo mwenye uwezo wa kuipeleka timu kwenye kiwango cha juu zaidi huku akibeba majukumu ya kizazi kipya katika eneo la kiungo.