Ratiba ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya NBC msimu mpya umekamilika, huku vigogo wa soka Tanzania, Simba SC na Yanga SC, wakianza kampeni zao za kusaka ubingwa kwa mechi za ugenini.
Mabingwa watetezi Yanga SC wataanza msimu mpya Agosti 15 kwa kuvaana na Namungo FC katika Uwanja wa Majaliwa, Lindi, wakilenga kuanza vyema harakati za kutetea taji lao.
Kwa upande wa Simba SC, Wekundu wa Msimbazi watashuka dimbani Agosti 16 dhidi ya Kagera Sugar katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, wakisaka pointi tatu za kwanza zitakazowaweka kwenye njia ya kuwania ubingwa.
Ratiba hiyo inaashiria mwanzo wa msimu mpya wenye ushindani mkubwa, huku kila timu ikitamani kuanza kwa ushindi ili kujijengea morali mapema katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC.