Local,Normal News,Local,Normal News,TPLB, NBC Premier League

TPLB yafafanua sababu ya kutoa ratiba ya Ligi Kuu ya NBC mapema

Jairo Mtitu By Jairo Mtitu
20 Jul 2026
TPLB yafafanua sababu ya kutoa ratiba ya Ligi Kuu ya NBC mapema

Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Cornel Barnabas, amesema uamuzi wa kutoa mapema ratiba ya Ligi Kuu ya NBC msimu mpya umefanyika kwa lengo la kuzipa klabu muda wa kutosha kufanya maandalizi ya kiufundi na kiutawala kabla ya kuanza kwa mashindano.

Kwa upande mwingine Barnabas amesema hatua hiyo itawezesha timu kupanga mipango yao mapema ikiwemo maandalizi ya programu za mazoezi, safari za michezo ya ugenini pamoja na mikakati ya benchi la ufundi kuelekea kila mchezo.

Pia ameongeza kwa kusema, TPLB imeendelea kuboresha mifumo ya uendeshaji wa ligi kwa kuhakikisha wadau wote wanapata taarifa muhimu kwa wakati, jambo ambalo linaongeza ufanisi na ushindani ndani ya Ligi Kuu ya NBC.

“Ratiba inapotolewa mapema, kila klabu inapata nafasi ya kupanga vizuri mambo yake. Tunataka kuona timu zinashiriki ligi zikiwa zimejiandaa kikamilifu na mashabiki nao waweze kupanga mapema kufuatilia michezo yao,” amesema Barnabas.

Kwa mujibu wa Afisa huyo, utoaji wa ratiba mapema pia unalenga kupunguza changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza katika misimu iliyopita, hususan upande wa maandalizi ya timu, usafiri na mipangilio ya mechi.

Ameongeza kuwa TPLB itaendelea kushirikiana na klabu, wadau wa soka pamoja na mamlaka mbalimbali kuhakikisha msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC unakuwa na ushindani mkubwa, uwazi na viwango bora zaidi.

Msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC unatarajiwa kuanza huku vilabu vikubwa nchini vikiendelea kukamilisha usajili na maandalizi ya vikosi vyao kwa ajili ya kuwania mafanikio katika mashindano ya ndani na kimataifa.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE →
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE →
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE →
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE →
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE →
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE →
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE →
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE →
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE →
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
23h ago
READ MORE →