Local,Transfer News,Simba Sc, TRA

Mpango wa Chobwedo kutua Simba wakwama, sababu yatajwa

Joel JJ By Joel JJ
β€’
20 Jul 2026
Mpango wa Chobwedo kutua Simba wakwama, sababu yatajwa

Ndoto ya winga mahiri wa TRA United, Ramadhan Chobwedo, kujiunga na Simba SC katika dirisha hili la usajili imegonga mwamba baada ya changamoto ya majeraha iliyompata kuelekea mwisho wa msimu uliopita.

Taarifa zinaeleza kuwa Chobwedo alikuwa amefikia makubaliano ya awali ya kutua Msimbazi mara baada ya msimu kumalizika. Hata hivyo, mipango hiyo imesimama kufuatia jeraha alilopata ambalo linatarajiwa kumuweka nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.

Inaelezwa kuwa winga huyo alipata majeraha katika mechi za mwisho za msimu, huku ripoti zikionyesha atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki 12 ili kuendelea na matibabu na programu ya kurejea katika kiwango chake.

Ni pigo kubwa kwa Chobwedo ambaye alikuwa katika kiwango bora msimu uliopita na kuvutia vilabu kadhaa, huku Simba ikionekana kuwa ndiyo iliyokuwa mbele katika mbio za kupata saini yake. Majeraha hayo yamekatisha kwa muda ndoto yake ya kuvaa jezi ya Wekundu wa Msimbazi.

Kwa sasa, nyota huyo anaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa wataalamu, huku ikielezwa kuwa endapo ataendelea vizuri na programu ya kupona, anaweza kurejea uwanjani mwanzoni mwa mwaka 2027.

Simba, kwa upande wake, inalazimika kuendelea kutafuta mbadala katika eneo la ushambuliaji katika kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya wa mashindano.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
5h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
9h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
12h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
14h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
15h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
15h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
21h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’