Local,Transfer News,Yanga, Azam, Simba NBC, CRDBankFederationCup

Kwisha habari yenu, Yanga yamtambulisha Mtaalamu wa mipira ya kutenga

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
21 Jul 2026
Kwisha habari yenu, Yanga yamtambulisha Mtaalamu wa mipira ya kutenga

Klabu ya Yanga SC imemkaribisha rasmi Kagisho Dikgacoi, kocha mwenye asili ya Afrika Kusini, kuwa sehemu ya kikosi cha ufundi cha kocha mkuu mpya Manqoba Mngqithi, akichukua jukumu la kocha wa mipira ya kutenga (Set Piece Coach). Dikgacoi ni miongoni mwa timu ya kiufundi ya Afrika Kusini iliyowasili Jangwani kufuatana na Mngqithi.

Dikgacoi ana historia ndefu ya soka nchini Afrika Kusini, akiwa aliwahi kucheza kwa timu za Golden Arrows, Fulham, Crystal Palace na Cardiff City, huku pia akiwa mchezaji wa kimataifa aliyecheza mechi 54 kwa Timu ya Taifa ya Bafana Bafana. Kabla ya kujiunga na Yanga, alikuwa msaidizi wa kocha katika klabu ya Golden Arrows, akifanya kazi bega kwa bega na Mngqithi.

Kuwasili kwake kunaendana na mkakati wa Mngqithi wa kuleta timu yenye uzoefu wa kimataifa kutoka PSL, ikiwemo pia wataalamu wengine kama Simo Dladla na mchambuzi wa utendaji Yardaan Valodia, huku lengo kuu likiwa ni kuiwezesha Yanga kuendelea kutawala ndani na kushindana vyema katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
5h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
8h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
12h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
14h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
15h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
15h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
20h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’