Klabu ya Yanga imeendelea kuonyesha nguvu zake katika dirisha la usajili kuelekea msimu wa 2026/2027 baada ya kukamilisha usajili wa beki wa kati Mohamed Mussa kutoka Mashujaa FC.
Mussa, ambaye ana umri wa miaka 22, amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga, huku akitarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya mabingwa hao wa Tanzania Bara katika msimu ujao.
Taarifa zinaeleza kuwa beki huyo aliamua kujiunga na Yanga licha ya kuvutiwa na ofa kutoka klabu nyingine kubwa, ikiwemo Azam FC, akichagua kuendeleza safari yake ya soka akiwa Jangwani.
Usajili wa Mohamed Mussa unamfanya kuwa mchezaji wa tatu kuhamia Yanga akitokea Mashujaa FC katika dirisha hili la usajili. Tayari klabu hiyo ilikuwa imewatambulisha mshambuliaji Hussein Mihambo pamoja na mlinzi wa pembeni Abdulnasir Gamal , ambao wote wametokea Mashujaa.


Hatua hiyo inaonyesha wazi imani ya Yanga kwa vipaji vilivyoibuliwa na Mashujaa FC, huku ikiongeza ushindani ndani ya kikosi kinachojiandaa kutetea mataji ya ndani na kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa msimu wa 2026/2027.