Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, ametoa pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA), Gianni Infantino, akisema ameendelea kuonyesha uaminifu na dhamira ya dhati katika kuisaidia Afrika kukuza mchezo wa soka.
Akizungumza kuhusu ushirikiano kati ya CAF na FIFA, Motsepe amesema Infantino amekuwa mstari wa mbele kuunga mkono maendeleo ya soka barani Afrika kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo, kuimarisha miundombinu, kuongeza uwekezaji na kutoa fursa zaidi kwa mataifa ya Afrika kushiriki katika mashindano ya kimataifa.
Motsepe amesema uhusiano wao wa kikazi umejengwa katika msingi wa kuheshimiana na kushirikiana, akisisitiza kuwa Infantino amekuwa mwaminifu si kwa Afrika pekee, bali pia kwake binafsi.
Ameeleza kuwa ushirikiano huo umechangia mafanikio makubwa ya soka la Afrika katika miaka ya hivi karibuni na unaendelea kufungua milango ya maendeleo zaidi kwa vyama na vilabu vya bara hilo.