Local,Transfer News,Wydad CA, Simba

Wydad yakanusha makubaliano na Simba kuhusu Mwalimu, yatoa vitisho

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Jul 2026
Wydad yakanusha makubaliano na Simba kuhusu Mwalimu, yatoa vitisho

Saa chache baada ya Klabu ya Simba SC kutangaza kufikia makubaliano ya kumuongezea mkataba wa mkopo mshambuliaji Selemani Mwalimu, Wydad Athletic Club (Wydad AC), wameibuka na kukanusha taarifa hizo huku wakitishia kuchukua hatua kali za kisheria.

Katika taarifa rasmi iliyotolewa na Wydad kupitia kurasa zao za kijamii, miamba hiyo ya Casablanca imebainisha kuwa hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa kati yao na Simba kuhusu mchezaji huyo, na kwamba taarifa zilizosambazwa na si za kweli.

Wydad imesisitiza kuwa Selemani Mwalimu bado ni mchezaji wao halali kisheria na yumo kwenye mipango ya benchi la ufundi kwa ajili ya msimu ujao, hivyo anapaswa kurejea kikosini haraka iwezekanavyo.

"Uongozi wa Wydad Athletic Club unapenda kuufahamisha umma na mashabiki kuwa taarifa zinazosambazwa na Klabu ya Simba kuhusu makubaliano mapya ya Selemani Mwalimu si za kweli. Hatujasaini mkataba wowote na klabu hiyo," ilieleza sehemu ya taarifa ya miamba hiyo ya Morocco.

Aidha, Wydad imeongeza kuwa itawasilisha malalamiko rasmi kwenye Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) pamoja na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) dhidi ya Simba SC kwa kile walichokiita ni ukiukwaji wa taratibu za usajili na upotoshaji wa makusudi unaolenga kuchafua taswira ya klabu hiyo.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
5h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
8h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
12h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
14h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
15h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
15h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
20h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’