Waamuzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wameingia katika awamu ya tano ya mafunzo ya matumizi ya teknolojia ya Video Assistant Referee (VAR), ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea matumizi rasmi ya mfumo huo katika soka la Tanzania. Mafunzo hayo yanaendelea chini ya usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), likiongozwa na Rais wake, Wallace Karia.





