Klabu ya Zamalek ya Misri imepiga hatua kubwa katika jitihada za kuondolewa marufuku ya usajili iliyowekwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), baada ya kupunguza idadi ya kesi za kifedha zinazoikabili kutoka 18 hadi tano. Hatua hiyo imekuja kufuatia klabu hiyo kufanikiwa kumaliza migogoro kadhaa iliyokuwa ikihusisha madeni ya wachezaji, makocha wa zamani na vilabu mbalimbali.





