Kiungo mshambuliaji Ladark Chasambi ameanza maisha mpya kunako klabu ya Singida BS baada ya kukamilisha usajili wake akitokea klabu ya Simba.
Chasambi amejiunga na matajiri hao wa Singida katika dirisha hili baada ya kumaliza mkataba na klabu ya Simba.
Nyota huyo amejumuishwa kwenye kikosi cha Singida BS kilichoweka kambi nchini Rwanda kushiriki mchuano ya CECAFA Kagame Cup inayotarajiwa kuanza leo nchini Rwanda.
Chasambi ni miongoni mwa wachezaji wanaotizamwa kuwa na vipaji vikubwa hata hivyo hakuwa na wakati mzuri alipokuwa na klabu ya Simba.
Singida BS wamemuhakikishia kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara wakitambua ubora wake.