Local,Transfer News,Simba

Simba yamtambulisha Doumbia, mfungaji bora ligi kuu Mali

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Jul 2026
Simba yamtambulisha Doumbia, mfungaji bora ligi kuu Mali

Klabu ya Simba SC imeendelea kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya baada ya kumtambulisha rasmi mshambuliaji Ibrahim Doumbia (22), ambaye anajiunga na Wekundu wa Msimbazi akitokea klabu ya AS Korofina ya nchini Mali.

Kwa mujibu wa taarifa, Doumbia amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka wa pili kulingana na makubaliano ya pande zote.

Mshambuliaji huyo ametua Msimbazi kama mchezaji huru baada ya kumalizika kwa mkataba wake na AS Korofina, hatua inayoipa Simba huduma za mmoja wa washambuliaji waliokuwa moto zaidi katika soka la Mali msimu uliopita.

Alitamba Ligi Kuu ya Mali

Doumbia anawasili akiwa na rekodi ya kuvutia baada ya kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Mali msimu uliopita.

Akiitumikia AS Korofina, nyota huyo alifunga mabao 17 katika michezo 24 ya ligi, akiongoza chati ya wafungaji na kuvutia vilabu mbalimbali barani Afrika kutokana na kiwango chake bora.

Mbali na mabao hayo, Doumbia alitoa pasi nne za mabao (assists), akionyesha uwezo wake wa kutengeneza nafasi kwa wenzake sambamba na kumalizia mashambulizi.

Aliangaza pia Kombe la FA

Mbali na mafanikio yake kwenye ligi, mshambuliaji huyo pia alifanya vizuri katika michuano ya Kombe la FA nchini Mali, ambapo alifunga mabao manne na kumaliza katika nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji bora wa mashindano hayo.

Takwimu hizo zinathibitisha uwezo wake wa kufunga katika mashindano tofauti na kumfanya kuwa mmoja wa washambuliaji waliokuwa kwenye kiwango bora zaidi nchini Mali msimu uliopita.

Usajili wa Doumbia ni sehemu ya mkakati wa Simba wa kuimarisha kikosi kuelekea Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho la CRDB pamoja na michuano ya CAF msimu ujao.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’