Local,Transfer News,Yanga Sc

Silaha tatu za moto zilizoshushwa na Yanga, Injinia Hersi akitangaza

Joel JJ By Joel JJ
25 Jul 2026
Silaha tatu za moto zilizoshushwa na Yanga, Injinia Hersi akitangaza

Rais wa Klabu ya Young Africans (Yanga SC), Injinia Hersi Said, usiku wa Ijumaa Julai 24, 2026, amewalipua mashabiki wa klabu hiyo kwa kutambulisha rasmi wachezaji watatu wapya wa kimataifa, huku akiahidi kuwa huu ni mwanzo tu wa mapinduzi makubwa ya kikosi hicho kuelekea msimu wa 2026/2027.

Utambulisho huo uliorushwa mubashara kupitia Runinga ya Azam TV na mitandao ya kijamii ya klabu, unahusisha wachezaji watatu kati ya watano wa kigeni ambao Yanga imewasajili kwa siri kubwa kuimarisha safu yake ya ushambuliaji na kiungo.

Mashine Mpya ya Mabao yashushwa

Katika utambulisho huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu, Yanga imemshusha mshambuliaji hatari raia wa Senegal mwenye asili ya Ufaransa, Cheick Ibrahima Touré, akitokea nchini Saudi Arabia.

Touré amesaini mkataba wa miaka miwili na ametajwa na Injinia Hersi kama "Mashine ya Mabao" (Goal Machine) itakayokuja kutatua changamoto za ufungaji klabuni hapo.

Mbali na Touré, Yanga imekamilisha usajili wa winga machachari wa kushoto kutoka nchini Zambia, Albert Kangwanda, ambaye anasifika kwa kasi na chenga za kuudhi, akiwa ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora (MVP) nchini mwao msimu uliomalizika.

Mchezaji wa tatu aliyetambulishwa kukamilisha idadi hiyo ni nyota wa kimataifa, winga Housseine Zakouani kutoka Comoros., anayekuja kuongeza nguvu na uzoefu kwenye kikosi hicho.

Kauli ya Rais Hersi Said

Akizungumza wakati wa utambulisho huo, Injinia Hersi Said amewatoa hofu mashabiki wa Yanga na kusisitiza kuwa usajili huu umefanyika kwa umakini mkubwa kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi.

"Tunaingia kwenye msimu mpya tukiwa na malengo makubwa zaidi, si tu kutetea mataji yetu ya ndani, bali kufika mbali zaidi kimataifa. Wachezaji hawa watatu ni sehemu ya mpango mkakati wa kuifanya Yanga kuwa tishio Afrika," alisema Injinia Hersi.

Hersi amesema bado wachezaji wawili ambao watatambulishwa siku chache zijazo akiamini usajili wa nyota hao utakwenda kuongeza ubora wa kikosi na kuhakikisha wanafikia malengo ya kutwaa mataji yote ya ndani msimu ujao na kufanya vyema kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL)

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
6h ago
READ MORE →
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
10h ago
READ MORE →
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
11h ago
READ MORE →
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
13h ago
READ MORE →
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
16h ago
READ MORE →
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
16h ago
READ MORE →
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
16h ago
READ MORE →
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
18h ago
READ MORE →
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
22h ago
READ MORE →
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE →