Local, Tanzania

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Wanawake Afrika (WAFCON 2026) inaanza rasmi nchini Morocco

Jairo Mtitu By Jairo Mtitu
β€’
26 Jul 2026
Michuano ya Kombe la Mataifa ya Wanawake Afrika (WAFCON 2026) inaanza rasmi nchini Morocco

Pazia la michuano ya Kombe la Mataifa ya Wanawake Afrika (WAFCON 2026) linafunguliwa rasmi nchini Morocco, huku mataifa 16 yakijiandaa kuwania taji la ubingwa wa Afrika kwa upande wa wanawake.

Michuano hiyo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na uwepo wa timu zenye historia na ubora mkubwa katika soka la wanawake barani Afrika, huku macho yakiwa kwa mabingwa watetezi, wenyeji Morocco pamoja na mataifa mengine yenye nguvu kama Nigeria, Afrika Kusini, Zambia, Ghana na Cameroon.

Katika ratiba ya hatua ya makundi, Algeria itaanza kampeni dhidi ya Senegal siku ya Jumapili Julai 26 saa 2:00 usiku, kabla ya wenyeji Morocco kushuka dimbani dhidi ya Kenya saa 5:00 usiku.

Timu ya taifa ya Tanzania, Twiga Stars, itaanza safari yake ya kusaka mafanikio katika michuano hiyo Jumatatu Julai 27 dhidi ya Afrika Kusini, mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa timu zote mbili.

Mbali na mchezo huo, Ivory Coast itakutana na Burkina Faso katika siku hiyo hiyo, huku siku zinazofuata mashabiki wakitarajia kuona michezo mingine mikubwa ikiwemo Zambia dhidi ya Misri, Nigeria dhidi ya Malawi, Ghana dhidi ya Cape Verde pamoja na Cameroon dhidi ya Mali.

Michuano hiyo pia itashuhudia mechi kubwa katika hatua ya makundi, ikiwemo Senegal dhidi ya Kenya na Morocco dhidi ya Algeria, huku kila timu ikipambana kupata nafasi ya kufuzu hatua inayofuata.

WAFCON 2026 imeendelea kuwa jukwaa muhimu la kukuza soka la wanawake Afrika, huku wachezaji wakitumia michuano hiyo kuonyesha vipaji vyao na kuwania nafasi za kuwakilisha nchi zao katika mashindano makubwa ya kimataifa.

Kwa Tanzania, matumaini makubwa yanaelekezwa kwa Twiga Stars kuhakikisha wanafanya vizuri dhidi ya wapinzani wao na kuandika historia mpya katika michuano hiyo ya wanawake Afrika.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
5h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
8h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
12h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
14h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
15h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
15h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
20h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’