Real Madrid wamefikia makubaliano kamili na RB Leipzig ya kumsajili winga wa kimataifa wa Ivory Coast, Yan Diomande, katika usajili unaokadiriwa kuzidi β¬100 milioni.
Makubaliano hayo yamekamilika usiku huu, huku Diomande akitarajiwa kusafiri kuelekea jijini Madrid ndani ya wiki hii kwa ajili ya vipimo vya afya kabla ya kusaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo hadi Juni 2031.
Nyota huyo amekuwa mmoja wa wachezaji waliovutia zaidi barani Ulaya kutokana na kasi, uwezo wa kupiga chenga na mchango wake mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya RB Leipzig, hali iliyowafanya Real Madrid kuharakisha mazungumzo ili kuhakikisha wanamnasa kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Usajili wa Diomande unaendelea kuonyesha mkakati wa Real Madrid wa kuwekeza kwa wachezaji vijana wenye vipaji vikubwa, huku akitarajiwa kuongeza ushindani katika safu ya ushambuliaji ya miamba hiyo ya Hispania.
DONE DEAL! Yan Diomande ni mchezaji mpya wa Real Madrid, akisubiri tu kukamilisha vipimo vya afya na kusaini mkataba wake rasmi.Β