Beki wa kati na nahodha msaidizi wa Yanga Dickson Job 'BBD' anazidi kuimarika katika program ya recovery anayoendelea nayo.
Job amekosekana uwanjani kwa takribani miezi minne, baada ya kupona majeraha sasa ameanza mazoezi ya 'fitness'. Ni hatua muhimu kuelekea kurejea kwenye majukumu yake.
Job pamoja na mshambuliaji Clement Mzize ambao wote walikuwa nje kwa muda mrefu, wamejumuishwa kwenye program za mazoezi katika pre-season ya Yanga inayoendelea Avic Town ingawa Mzize huenda akawahi zaidi kurejea kikosini.
Mzize ameanza kushiriki mazoezi ya timu baada ya kuonyesha kuimarika haraka ingawa kulingana na Meneja wa Habari na Mawasiliano Ali Kamwe, bado atahitaji wiki kadhaa kuimarisha fitness yake kabla ya kuanza rasmi 'kukiwasha' kwenye mechi za ushindani
