Klabu ya Azam FC imeanza rasmi maandalizi ya msimu wa 2026/27 baada ya wachezaji na benchi la ufundi kuripoti kambini kwa mazoezi ya kwanza kuelekea kampeni mpya. Mazoezi hayo yamejikita katika kuimarisha utimamu wa mwili pamoja na maandalizi ya kiufundi, huku kocha mkuu akiongoza vikao vya awali na kutoa maelekezo kwa kikosi chake.
Maandalizi hayo yanafanyika wakati Azam FC ikiendelea kufanya maboresho ya kikosi kuelekea msimu mpya, ambapo timu hiyo imefanya sajiri Mbalimbali kubwa ikiwemo kumrejesha nyota wa zamani wa Timu hiyo Kipre Jr.
Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC itaanza kampeni ya msimu wa 2026/27 kwa mchezo wa ugenini dhidi ya Polisi Tanzania utakaochezwa Agosti 15, 2026.