Meneja habari na mawasiliano wa klabu ya yanga Ally Kamwe ametanabaisha kuwa wachezaji wa klabu hiyo ambao walikuwa majeruhi Dickson Job na Climent Mzize hali zao zimezidi kuimarika kwa kasi tofauti na mategemeo yao .
Ally amesema hayo hii leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Timu hiyo jangwani jijini Dar es salaam .
" Ripoti ya daktari aliyonipa mara ya mwisho ilionesha hivi Vyuma vinarudi uwanjani December lakini Mzize na Job ni Extraordinary , Mwezi wa kumi wamo " Kamwe alisema
Mzize na Job wamekosekana katika kikosi Cha yanga tokea msimu uliomalizika ambapo Mzize alipata jeraha lake katika mchezo dhidi ya Walliete kuwania kufuzu makundi ligi ya Mabingwa na Job dhidi ya Simba katika fainali ya Muungano