Meneja habari na mawasiliano wa klabu ya yanga Ally Kamwe ametanabaisha kuwa wachezaji wa klabu hiyo ambao walikuwa majeruhi Dickson Job na Climent Mzize hali zao zimezidi kuimarika kwa kasi tofauti na mategemeo yao .
Ally amesema hayo hii leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Timu hiyo jangwani jijini Dar es salaam .





