Klabu ya Young Africans (Yanga) ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa kiungo mkabaji Fred Ngoma kutoka Olympique De Safi ya Morocco. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 na raia wa Congo Brazzaville anatajwa kuwa amekubaliana na Yanga kuhusu masharti yote binafsi, huku akisubiriwa kuwasili nchini kukamilisha taratibu za mwisho za uhamisho wake.





