Klabu ya Polisi Tanzania imekamilisha usajili wa kipa Beno David Kakolanya kuelekea msimu wa 2026/27 wa Ligi Kuu ya NBC.
Kakolanya, mwenye umri wa miaka 32, anajiunga na Maafande hao akitokea Mbeya City baada ya kusaini mkataba rasmi wa kuitumikia klabu hiyo.



