Kiungo mshambuliaji kutoka Afrika Kusini, Neo Maema, amerejea rasmi Simba SC kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea klabu ya Mamelodi Sundowns, baada ya pande zote kufikia makubaliano ya uhamisho huo.
Uamuzi wa kumrejesha Maema umeungwa mkono na kocha mkuu Barker, ambaye anaamini kiungo huyo atakuwa sehemu muhimu ya kikosi chake kuelekea msimu wa 2026/27.





