Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza viingilio kwa mashabiki watakaoshuhuda mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC, mchezo unaotarajiwa kuzikutanisha timu hizo kongwe katika soka la Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF, mchezo huo utapigwa Jumatatu, August 12 kwenye uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar, saa 2:30 usiku





