Mashabiki wa Yanga ndio watu wenye furaha zaidi nchini baada ya usiku wa kuamkia leo wakiishuhudia timu yao ikitwaa Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani zao Simba katika mchezo uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.
Matukio mbalimbali ya shangwe la wachezaji wa Yanga na benchi la ufundi baada ya kutwaa taji hilo la kwanza msimu huu.





