Ligi Kuu ya NBC 2026/27 ilianza rasmi jana, huku ushindani wa msimu mpya ukiendelea leo Jumamosi kwa michezo mitatu baada ya mechi nyingine tatu kupigwa jana Ijumaa.
Msimu huu umeanza kwa matokeo yaliyotoa taswira ya ushindani unaotarajiwa, huku Yanga SC na Azam FC zikiwa miongoni mwa timu zitakazoshuka dimbani leo kuanza kampeni zao.





