Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ali, amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuhusu hali ya mlinda lango Djibrilla Kassali, ambaye alipata jeraha katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC.
Kassali alishindwa kuendelea na mchezo huo dakika ya 80 baada ya kupata jeraha kwenye msuli wa nyuma ya paja wakati akijaribu kuokoa hatari langoni.





