Hatma ya uhamisho wa Julián Alvarez imeendelea kutikisa Atletico Madrid, huku mshambuliaji huyo wa Argentina akihusishwa kwa nguvu na mpango wa kuhamia Barcelona.
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinaeleza kuwa Alvarez bado ana ndoto ya kujiunga na Barcelona, licha ya Atletico Madrid kuweka wazi kuwa hawana mpango wa kumuuza, hasa kwa klabu hiyo ya Catalunya.





