Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema klabu hiyo haina taarifa yoyote kuhusu madai yanayohusisha usajili wa Selemani Mwalimu kwenda Yanga SC.
Ahmed Ally amesema Simba haijui lolote kuhusu taarifa zinazodai kuwa Selemani Mwalimu anashindwa kuitumikia Yanga kutokana na Simba kugoma kumuondoa mchezaji huyo kwenye mfumo wa FIFA Connect.





