Manqoba akiri JKT Tanzania sio ya kubeza

Joel JJ By Joel JJ β€’ 23rd August 2026


Manqoba akiri JKT Tanzania sio ya kubeza

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi, ameitahadharisha timu yake kuelekea mchezo dhidi ya JKT Tanzania licha ya wapinzani wao kuwa na mwanzo usioridhisha katika msimu huu wa Ligi Kuu.

Manqoba amesema mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa kesho Jumatatu kwenye Uwanja wa KMC Complex unaweza kuwa mgumu zaidi ukilinganisha na michezo ambayo Yanga imecheza hadi sasa msimu huu.

Akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo, kocha huyo raia wa Afrika Kusini amesema matokeo ambayo JKT Tanzania imeyapata katika michezo yake miwili iliyopita hayatoi picha halisi ya uwezo wa kikosi hicho.

“Kwa mtazamo wangu naona JKT Tanzania ni timu nzuri sana. Nafikiri matokeo waliyopata katika mechi zilizopita hayaakisi ubora wa timu yao. Kocha Ahmed Ali amefanya kazi nzuri.”

Manqoba ameongeza kuwa JKT Tanzania ina wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi na kwamba timu hiyo inaonyesha dalili za kukua kwa kasi.

“Wana wachezaji wengi wabunifu, ni timu inayoonekana kukua haraka. Tunapaswa kwenda kuwakabili kwa umakini mkubwa,” alisema Manqoba.

Maandalizi mafupi, matumaini makubwa

Licha ya ratiba kuwa ngumu na kutokuwa na muda wa kutosha wa maandalizi, Manqoba amesema kikosi chake kiko tayari kupambana ili kuendeleza mwanzo mzuri wa msimu.

Kocha huyo amekiri kuwa Yanga bado haijafikia kiwango cha ubora anachokihitaji kutokana na muda mfupi wa maandalizi, lakini anaamini kikosi kitaendelea kuboresha kiwango kadiri msimu utakavyoendelea.

Manqoba pia amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa KMC Complex ili kuwapa hamasa wachezaji wake katika mchezo huo.

Amesema sapoti ya mashabiki ni sehemu muhimu ya kuwapa nguvu wachezaji, huku akiahidi kwamba vijana wake watapambana kuhakikisha wanaondoka na matokeo yatakayowafurahisha mashabiki wao.

Yanga bila Job na Mzize

Katika mchezo huo, Yanga itaendelea kuwakosa wachezaji wake wawili ambao bado wanaendelea na matibabu ya majeraha.

Manqoba amethibitisha kuwa Dickson Job na Clement Mzize hawatakuwepo kutokana na majeraha ya muda mrefu, lakini wachezaji wengine wote wako tayari kwa mchezo huo.


  

More Stories

Manqoba akiri JKT Tanzania sio ya kubeza
Manqoba akiri JKT Tanzania sio ya kubeza
Today, READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 20, August 23 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 20, August 23 2026
Today, READ MORE β†’
NBC Premier league, Michezo miwili kuendelea.
NBC Premier league, Michezo miwili kuendelea.
Today, READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Hizi hapa ni odds za uhakika, treni la wiki mbili
Xtra 90 Bets : Hizi hapa ni odds za uhakika, treni la wiki mbili
Today, READ MORE β†’
Mourinho aanza na alama tatu La Liga
Mourinho aanza na alama tatu La Liga
Today, READ MORE β†’
Geita Gold yamuangushia Kagera Sugar kipigo cha paka mwizi.
Geita Gold yamuangushia Kagera Sugar kipigo cha paka mwizi.
Today, READ MORE β†’
Highlights : Geita Gold 6-2 Kagera Sugar
Highlights : Geita Gold 6-2 Kagera Sugar
Today, READ MORE β†’
Simba yaendeleza ushindi wa asilimia 100 ugenini
Simba yaendeleza ushindi wa asilimia 100 ugenini
Today, READ MORE β†’
Simba bado nidhamu ya mchezo ipo chini, kadi nyekundu ya tatu mfululizo yawatokea
Simba bado nidhamu ya mchezo ipo chini, kadi nyekundu ya tatu mfululizo yawatokea
Today, READ MORE β†’
Highlights : Singida BS 1-2 Simba
Highlights : Singida BS 1-2 Simba
Today, READ MORE β†’