Kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salumu anatarajiwa kurejea kikosini apo kesho kufuatia kukosa Michezo mitatu ya msimu wa 2026-27 kutokana na kifungo Cha kadi nyekundu aliyoipata msimu wa 2025-26 fainali ya CRDB CUP dhidi ya Simba .
Feisal amekosa michezo dhidi ya Polisi Tanzania, TRA United na dhidi ya Pamba Jiji na atarejea apo kesho ambapo Azam FC itakuwa ugenini katika uwanja wa Bukombe dhidi ya Geita Gold.
Azam tayari imekusanya alama 7 kati ya 9 ambazo wamewania msimu huu baada ya kushinda miwili na Sare Moja dhidi ya Polisi Tanzania
Urejeo wa Feisal unaenda kuboresha eneo la ushambuliaji la Azam FC ambalo Limekwisha funga mabao 5 msimu huu wa 2026-27



