Simba yatakata Isamuhyo, yaichapa Coastal Union 1-0

Joel JJ By Joel JJ
•
27 Aug 2026
Simba yatakata Isamuhyo, yaichapa Coastal Union 1-0

Simba SC imeendeleza rekodi yake ya ushindi kwa asilimia 100 msimu huu baada ya kuichapa Coastal Union bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni jijini Dar es Salaam.

Ulikuwa mchezo ambao Simba ilitawala kwa muda mwingi, huku Wekundu wa Msimbazi wakimiliki mchezo na kutengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga ukilinganisha na wapinzani wao.

Katika kipindi cha kwanza, washambuliaji wa Simba walikosa umakini katika umaliziaji na kushindwa kutumia nafasi kadhaa za wazi walizozipata. Kwa upande wao, Coastal Union waliweka mkazo zaidi katika kujilinda na kuzuia mashambulizi ya Simba.

Baada ya mfululizo wa mashambulizi kwenye lango la Coastal Union, Simba hatimaye ilifanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 74 kupitia Ismail Touré, aliyemalizia kwa kichwa krosi nzuri ya Anicet Oura.

Katika dakika za lala salama, Simba ilipata mkwaju wa penalti baada ya Elie Mpanzu kuonekana kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari. Hata hivyo, baada ya tukio hilo kufanyiwa mapitio kupitia mfumo wa FVS, uamuzi wa kutoa penalti ulifutwa.

Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa Simba kuandikisha ushindi wake wa nne mfululizo msimu huu, huku ikirejea kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 12.

Ushindi huo unaifanya Simba kuendelea na mwanzo bora wa msimu, ikiwa bado haijapoteza mchezo wala kupoteza alama katika michezo yake minne ya kwanza.

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester City yaichapa Liverpool 3-0, Anderson aibuka mchezaji bora.
Manchester City yaichapa Liverpool 3-0, Anderson aibuka mchezaji bora.
8h ago
READ MORE →
Carrick kupewa mechi mbili kuokoa kibarua chake Manchester United.
Carrick kupewa mechi mbili kuokoa kibarua chake Manchester United.
10h ago
READ MORE →
EPL: Mechi za leo, Liverpool na Manchester City Kusaka mbabe
EPL: Mechi za leo, Liverpool na Manchester City Kusaka mbabe
17h ago
READ MORE →
Manqoba amtaja Abuya kipigo dhidi ya Simba
Manqoba amtaja Abuya kipigo dhidi ya Simba
19h ago
READ MORE →
Barcelona inagawa dozi tu La Liga, yaipiga Getafe 3-0
Barcelona inagawa dozi tu La Liga, yaipiga Getafe 3-0
20h ago
READ MORE →
Real Madrid yaishinda kwa tabu Villarreal, Vinícius Jr apewa kadi nyekundu
Real Madrid yaishinda kwa tabu Villarreal, Vinícius Jr apewa kadi nyekundu
21h ago
READ MORE →
Arsenal yaendeleza ubabe EPL, Manchester United yavutwa shati na Spurs pungufu
Arsenal yaendeleza ubabe EPL, Manchester United yavutwa shati na Spurs pungufu
21h ago
READ MORE →
Simba ingeongeza umakini, tungeifunga Yanga mabao 10 - Mangungu
Simba ingeongeza umakini, tungeifunga Yanga mabao 10 - Mangungu
1d ago
READ MORE →
Simba yamaliza uteja dhidi ya Yanga, yashinda dabi na swaga
Simba yamaliza uteja dhidi ya Yanga, yashinda dabi na swaga
1d ago
READ MORE →
Highlights : Simba 2-1 Yanga
Highlights : Simba 2-1 Yanga
1d ago
READ MORE →