Kocha Simba amtetea Doumbia, atafunga sana

Joel JJ By Joel JJ • 28th August 2026

Kocha Simba amtetea Doumbia, atafunga sana

Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker, amemtetea mshambuliaji Ibrahim Doumbia baada ya kukosa kutumia baadhi ya nafasi alizopata katika mchezo dhidi ya Coastal Union, akisisitiza kuwa hana wasiwasi na uwezo wa nyota huyo kufunga mabao mengi msimu huu.

Simba ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, huku Doumbia akipata nafasi kadhaa za kufunga lakini akashindwa kuzitumia ipasavyo.

Licha ya kutofunga, Barker amesema mshambuliaji huyo alifanya kazi kubwa uwanjani na kwamba alikosa bahati ya kuweka mpira kambani.

“Doumbia ni mshambuliaji mzuri, sisi tunamuamini. Nafikiri leo alikosa bahati tu ya kufunga, lakini amefanya jitihada kubwa uwanjani,” alisema Barker.

Kocha huyo ameongeza kuwa hali hiyo ni ya kawaida kwa mchezaji mpya, akieleza kuwa Doumbia bado anahitaji muda wa kuzoea mazingira mapya pamoja na mfumo wa uchezaji wa Simba.

“Hii ni hali ya kawaida kwa mchezaji mgeni. Anahitaji kuzoea mazingira pamoja na mfumo wetu wa uchezaji kwa ujumla.”

Barker amesema hana mashaka na uwezo wa mshambuliaji huyo na anaamini muda si mrefu ataanza kuonyesha makali yake mbele ya lango.

“Sina wasiwasi naye, ni mchezaji mzuri. Ninaamini atatufungia mabao mengi msimu huu,” alisema Barker.

Wakati huo huo, mashabiki wa Simba wamehimizwa kuendelea kumpa Doumbia sapoti na kumvumilia katika kipindi hiki cha mwanzo, ili kumpunguzia presha na kumpa nafasi ya kuzoea mazingira na mfumo wa timu.

More Stories

Alvarez akosa mazoezi siku tatu katika sakata la kuhama
Alvarez akosa mazoezi siku tatu katika sakata la kuhama
Today, READ MORE →
Rafael Leão Ajiunga na Aston Villa kwa Mkopo.
Rafael Leão Ajiunga na Aston Villa kwa Mkopo.
Today, READ MORE →
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 16, August 28 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 16, August 28 2026
Today, READ MORE →
Kocha Simba amtetea Doumbia, atafunga sana
Kocha Simba amtetea Doumbia, atafunga sana
Today, READ MORE →
Barcelona yaichapa Athletic Club 2-0, yarudi kileleni La Liga
Barcelona yaichapa Athletic Club 2-0, yarudi kileleni La Liga
Today, READ MORE →
Mwalimu ruksa kuitumikia Yanga, ITC yake yatumwa TFF
Mwalimu ruksa kuitumikia Yanga, ITC yake yatumwa TFF
Today, READ MORE →
Simba yatakata Isamuhyo, yaichapa Coastal Union 1-0
Simba yatakata Isamuhyo, yaichapa Coastal Union 1-0
Today, READ MORE →
Highlights : Simba 1-0 Coastal Union
Highlights : Simba 1-0 Coastal Union
Today, READ MORE →
Fei toto kurejea kesho dhidi ya Geita Gold
Fei toto kurejea kesho dhidi ya Geita Gold
Yesterday, READ MORE →
Yaya Touré Aandika Historia UEFA Champions League, Awa mwafrika wa kwanza kufika hatua hii
Yaya Touré Aandika Historia UEFA Champions League, Awa mwafrika wa kwanza kufika hatua hii
Yesterday, READ MORE →