Yanga yaichapa Pamba Jiji 2-0, yarudi kileleni

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 Aug 2026
Yanga yaichapa Pamba Jiji 2-0, yarudi kileleni

Yanga SC imeendeleza ubabe wake katika Ligi Kuu ya NBC baada ya kuichapa Pamba Jiji mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex.

Zilikuwa dakika 90 za ushindani mkubwa kwa Pamba Jiji, ambao walionekana kupata wakati mgumu kuhimili mashambulizi ya Yanga. Hata hivyo, mlinda lango wao alifanya kazi kubwa kwa kuokoa michomo kadhaa na kuzuia timu yake kuondoka na kapu la mabao.

Yanga ilipata mabao yake yote mawili katika kipindi cha kwanza. Mshambuliaji Cheick Ibrahima Toure alihusika katika bao la kwanza baada ya kutoa pasi iliyomwezesha Maxi Nzengeli kufunga.

Toure hakukomea hapo, kwani alirejea mwenyewe kwenye ubao wa matokeo kwa kufunga bao la pili baada ya kumalizia krosi nzuri iliyopigwa na Peter Shalulile.

Kipindi cha pili Yanga iliendelea kutawala mchezo na kupata nafasi kadhaa za kuongeza mabao. Hata hivyo, uimara wa mlinda lango wa Pamba Jiji pamoja na kutokuwa makini kwa washambuliaji wa Yanga uliwazuia Wananchi kupata ushindi mkubwa zaidi.

Mshambuliaji Seleman Mwalimu aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Toure na alipata nafasi mbili nzuri za kufungua akaunti yake ya mabao, lakini hakufanikiwa kuzitumia.

Licha ya kutopata mabao zaidi, Yanga imeondoka na pointi zote tatu muhimu ambazo zimeirejesha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Ushindi huo unaendelea kuonyesha ubora wa safu ya ushambuliaji ya Yanga, huku mabingwa hao wakijipambanua kwa uwezo wao wa kufunga mabao mengi katika ligi.

ADVERTISE HERE

More Stories

Simba yaichakaza Mashujaa 6-1, Mpanzu atupia mawili.
Simba yaichakaza Mashujaa 6-1, Mpanzu atupia mawili.
57m ago
READ MORE β†’
Highlights : Simba 6-1 Mashujaa Fc
Highlights : Simba 6-1 Mashujaa Fc
1h ago
READ MORE β†’
Ally Kamwe awaomba Wanayanga subira, asema maoni yao yatafanyiwa kazi
Ally Kamwe awaomba Wanayanga subira, asema maoni yao yatafanyiwa kazi
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yapata pigo, Abuya nje wiki mbili hadi tatu
Yanga yapata pigo, Abuya nje wiki mbili hadi tatu
9h ago
READ MORE β†’
Israel Mwenda karibu kurejea Yanga baada ya Kutatuliwa kwa sakata lake
Israel Mwenda karibu kurejea Yanga baada ya Kutatuliwa kwa sakata lake
9h ago
READ MORE β†’
Kipigo cha Simba si mwisho, lengo letu ni Ubingwa: Ally Kamwe
Kipigo cha Simba si mwisho, lengo letu ni Ubingwa: Ally Kamwe
10h ago
READ MORE β†’
Mechi zote za 15 de Agosto na Simba SC kuchezwa Dar es Salaam
Mechi zote za 15 de Agosto na Simba SC kuchezwa Dar es Salaam
11h ago
READ MORE β†’
Ligi ya mabingwa Ulaya: United, Barca, Arsenal, Bayern mzigoni leo
Ligi ya mabingwa Ulaya: United, Barca, Arsenal, Bayern mzigoni leo
11h ago
READ MORE β†’
Simba kurejea uwanjani leo kuivaa Mashujaa NBC Premier League.
Simba kurejea uwanjani leo kuivaa Mashujaa NBC Premier League.
12h ago
READ MORE β†’
Coastal Union yaendeleza ubabe wa nyumbani, yaichapa Singida Black Stars
Coastal Union yaendeleza ubabe wa nyumbani, yaichapa Singida Black Stars
1d ago
READ MORE β†’